Mawakili wawili tegemeo waliokuwa wakimtetea Mchungaji tata, Paul Mackenzie na washukiwa wenzake kwenye tuhuma za kusababisha vifo vya mamia ya watu katika msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi wamejiondoa kwenye kesi hiyo.

Mawakili George Kariuki na Elisha Komora wamejiondoa wakisema hawawezi tena kuwakilisha wateja wao, wakisema mbele ya Mahakama ya Shanzu bila kufafanua kuwa wanakwamishwa, kupokea vitisho na wanahangaishwa.

Katika kesi hiyo iliyosomwa hii leo Juni 14, 2023, mbele ya Mahakama imefahamishwa kuwa wafuasi 16 wa mafundisho ya mhubiri huyo Paul Mackenzie waligoma kula tangu Juni 4, 2023.

Kiongozi wa Mawakili wa Upande wa Mashtaka Jami Yamina amesema ni Mackenzie tu na mshukiwa Smart Mwakalama ambao wamekuwa wakipata mlo.

Washukiwa wengine waliosalia walianza mgomo wa kususia mlo siku 10 zilizopita (tangu Juni 4, 2023) ambapo wamekataa kula chakula na kunywa maji.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 15, 2023
Kenya: Idadi ya waliofariki mfungo tata yafikia watu 303