Waziri wa fedha na mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba ameomba kuongeza Ushuru wa Barabara na Mafuta kwa kiasi cha shilingi 100 kwa kila lita ya mafuta ya Petroli na Dizeli.

Mwigulu ameyabainisha hayo Bungeni jijini Dodoma, na kuongeza kuwa Serikali pia inapendekeza kufanya marekebisho kwenye kifungu cha 4A cha Sheria ya Ushuru wa Barabara SURA, 220 kwa kuongeza kipengele ‘C’.

Amesema, “kipengele hicho kitakachoelekeza fedha zitakazokusanywa kutokana na ongezeko hili la ushuru wa barabara na mafuta la shilingi 100 kwa mafuta ya petroli na dizeli zitumike kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati iIi kupata vyanzo vya uhakika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.”

Hatua hii inatarajia kuongeza Mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 381,826.8 huku pia Serikali ikitarajia kuongeza kiwango Cha Kutoza Ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 20 kwenye mashine za Kamari zinazoingizwa kutoka nje ya nchi na zinazozalishwa nchini.

Cedric Kaze aigomea Young Africans
Mkutano EITI: Rais Samia ataka uwekezaji wenye manufaa