Wababe wa Kaskazini mwa jijini London ‘Arsenal’ wameripotiwa kutokuwa na mpango wa kumsajili kiungo kutoka Ecuador na klabu ya Brighton Moises Caicedo.

Kwa mujibu wa ripoti, The Gunners ambao walimaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Englang msimu uliopita walipania kumsajili kiungo huyo mwenye thamani ya Pauni 80 milioni.

Klabu hiyo ina lengo la kumsajili kiungo wa West Ham, Declan Rice ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa Pauni 100 milioni.

Juma lililopita, Hammers walikataa ofa ya Arsenal ya Pauni 80 milioni pamoja na nyongeza, sasa Mikel Arteta anajipanga kutuma ofa nyingine.

Taarifa ilivyoripotiwa na gazeti la Times ni kwamba Arsenal, imejiondoa cha kuwania saini ya Caicedo anayeelekea Chelsea.

Tayari Brighton imemuuza Alexis Mac Allister kwa Pauni 35 milioni kwenda Liverpool huku kiungo huyo wa kimataifa Ecuador akikaribia kutua Stamford Bridge.

Wakati huo huo, mabingwa wa ligi Man City wameibuka wakitaka kuipiku Arsenal katika mbio za kumsajili Rice mwenye miaka 24.

Haa hivyo Arsenal ina nafasi nzuri ya kumsajili Rice kwasababu alionyesha nia ya kuelekea mitaa ya jiji la London kwa muda mrefu.

Rice alihusishwa na timu kibao kama Manchester United, Bayern Munich, na Chelsea, lakini wakajiondoa katika kinyanga’nyiro cha kuwania saini yake. West Ham inaamini kwamba Rice ana thamani ya Pauni 110 milioni.

Jude Bellingham: Ninamkubali sana Zidane
Murilo atoa onyo maandamano kwenda Ikulu