Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro amewatahadharisha wananchi kuhusu taarifa zinazozagaa kutoka kwa mtu mmoja kuwa kutakuwa na maandamano siku ya Jumatatu Juni 19, 2023 kwenda Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam.

Kamanda Muliro amesema kuwa taarifa ya mtu huyo anayodai kuwa aliifikisha Polisi, tayari amejibiwa kwa kuyapiga marufuku maandamano aliyokuwa anataka kuyaratibu.

”Tayri amekwisha shauriwa kama anajambo muhimu la masingi ambalo labda anataka lisikilizwe basi ameshauriwa atumie vyombo mbalimbali vya kisheria amabavyo anaweza kufika na kuwasilisha hoja zake bila maandamano ili haki zingine za wananchi za kufanya kazi wakiwa huru zisiingiliwe”

Jeshi la Polisi linaendelea kuwatahadharisha kutoshiriki Jeshi la Polisi linawatahadharisha watu kutoshiriki hicho kinachodaiwa maandamano na badala yake wanawahimiza kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii bila hofu

“Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kwa mtu au kundi la watu ambao limepanga kuzusha taharuki kwa kuzuia watu wengine kufanya kazi zaoeti tu kwasababu kutakuwa na maandamano,” amesema.

”Kuna njia nyingi za mtu kutaka kusikika au kufahamika kwa kufanya vitendo ambavyo wakati mwingine unajua labda wakati wake au mazingira yake sio sahahihi unaweza ukadhani unazitumia sheria ambazo ni sehemu ya haki yako lakini wakati huohuo ukajikuta wakati ukipambania kutekeleza au kupata fursa ya matumizi ya haki yako lakini pia haki yako sio kigezo cha kuingia au kuvunja haki za watu wengine

”Lakini pia sio sahihi kwasababu una haki fulani basi wewe ukilala asubuhi au usiku ukiamka unasema mimi nataka kuandamanaa lazima taratibu zifuatwe na sababu za msingi za kufanya hivyo ziwepo”amesema Muliro

Arsenal yapotezea usajili wa Caicedo
AFCON 2024 kuivurugia Liverpool 2023/24