Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS, kujitathmini katika utendaji wao wa kazi.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Juni 17, 2023 wakati wa utoaji wa gawio la Serikali na sherehe za miaka 25 ya Benki ya NMB.

Amesema, “kajitizame vizuri ndani ya shirika, wengine wote kajitizameni vizuri hii haina kurudi nyuma, kuna nitakayofuta, nitakayosaidia na nitakayoipa miongozo jinsi ya kujiendesha ili wote mfanye faida.”

“Nasubiri taarifa ya mwisho ya mashirika gani yanabaki na yapi yanaondoka na yapi yasaidiwe vipi kufanya biashara, sitaki kuona shirika linazorota halafu meneja anavaa suti nzuri mtaani,” amebainisha Rais Samia.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 18, 2023
Julio: Simba SC, Young Africans mjipange 2023/24