Mabingwa wa Soka nchini Hispania Real Madrid wanajiandaa kumpa Beki wa kushoto Ferland Mendy mkataba mpya baada ya kufurahishwa na ubora wake katika Mzunguuko wa pili wa msimu huu 2023/24.

Ripoti nchini Hispania zimedai Mkataba wa sasa wa Mendy unanalizika msimu wa majira ya joto wa 2025 na alitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mwaka huu baada ya kushindwa kuushawishi uongozi wa Madrid kuhusu ubora wake, licha ya uungwaji mkono wa kocha Carlo Ancelotti.

Ancelotti amewahi kumtaja Mendy kama beki wa kushoto bora zaidi duniani na inaaminika amekuwa akihimiza Madrid kumpa mkataba mpya Mfaransa huyo na kwa mujibu wa Marca sasa amekubaliwa matakwa yake.

Huku wakitajwa kutaka kumfuatilia Davies msimu huu wa majira ya joto, ripoti zinasema Madrid walibadili msimamo wao na sasa wako tayari kusubiri hadi mkataba wake utakapomalizika 2025 ili kumsajili kwa uhamisho huru.

Maofisa wa Madrid Madrid wako tayari kufungua mazungumzo na Mendy kuhusu kuongeza muda, ripoti imesema, ingawa wa Mendy zinakuja huku kukiwa na uvumi kwamba Madrid wanapunguza nia yao ya kutaka kumsajili beki wa kushoto wa FC Bayern Munich, Alphonso Davies ambaye ni kama Mendy anayekaribia kumaliza miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake. Habari za mkataba mpya makubaliano hayafikiriwi kuwa karibu wakati huu.

Serikali yapeleka somo la Kiingereza darasa la kwanza
Nunez akoleza moto Liverpool