Serikali nchini, imesema imeandaa hatua na mikakati madhubuti yenye kuibua fursa za miradi ya kijamii kwa wananchi ikiwemo kanuni na mwongozo wa biashara ya kaboni ikiwa ni njia mbadala ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yameelezwa hii leo Juni 19, 2023 na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Abdallah Hassan Mitawi wakati akifunga warsha ya siku moja baina ya wahariri wa vyombo vya habari na Menejimenti ya Ofisi hiyo iliyolenga kujenga uelewa kuhusu kanuni na mwongozo wa biashara ya kaboni.

Amesema, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoathiriwa na athatri za mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa isiyotabirika hali inayojidhihirisha kupitia matukio ya mvua zisizotabirika, ongezeko la joto, ukame na mafuriko, ambapo athari hizo zimeathiri sekta za kijamii na kiuchumi.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Abdallah Hassan Mitawi akiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Sarah Kibonde mara wakati wa warsha baina ya Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais na Wahariri wa vyombo vya habari iliyofanyika jijini Dar es Salaam Juni 19, 2023.

“Pamoja na changamoto zinazochangiwa na mabadiliko ya tabia nchi kumekuwa na fursa na jitihada mbalimbali ambazo zimechukuliwa na serikali ikiwa ni pamoja na mapitio ya sera, uandaaji wa kanuni, mikakati na miongozo ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi,” amesema Mitawi.

Aidha, amesema biashara ya kaboni ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani inayotekelezwa na nchi wanachama wa Maktaba wa Mabadiliko ya tabianchi, itifaki ya Kyoto na makubaliano ya Paris, ambapo Tanzania ni  mwanachama wa mikataba hiyo.

Jenerali Mukunda ashiriki ufunguzi ushirikiano imara Rwanda
Beki wa Uganda aiita mezani Azam FC