Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara amesema huwa haigizi anapolia wakati akiwasemea wanatarime juu ya masuala mbalimbali, bali ni hisia za kweli za kisiasa alizonazo katika kuhakikisha Taifa linakuwa na uwajibikaji wenye haki kwa jamii nchini.

Waitara ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano maalum na Dar24 Media jijini Dodoma na kuongeza kuwa wale wanaosema analia ili kutafuta huruma ya kupoteza jimbo hawana mantiki bali uzushi huo unafanywa na mpinzani wake (jina linahifadhiwa).

Amesema, “mtadanganywa sana kwenye vyombo hivi lakini mimi ni mtu ambaye napenda kwenda field na mimi nikiwa nafanya siasa huwa siigizi na huyo mpinzani wangu asithubutu kukanyaga kule atakiona, na stori zote hizi tukunate kule 2025,”

Aidha Waitara amesema Duniani watu wameumbwa tofauti na kutoa machozi ni moja ya jambo la kutafuta unafuu kwani kila mtu ana namna yake ya kupata ahueni au kufurahi ikiwemo kulia pale anapokabiliana na ugumu wa jambo liwe la kumuumiza au la kumpa furaha.

Jose Mourinho kutimkia Saudi Arabia
Simba SC yabisha hodi Vipers SC