Wakazi wa Murang’a nchini Kenya, wameitaka Serikali kuhakikisha inawajibika katika matumizi sahihi ya damu waliyoitoa kwa hiari, wakionya dhidi ya watendaji wasio waaminifu kugeuza hitaji hilo kuwa biashara.

Wakiongea mjini Murang’a katika hafla kuadhimisha siku ya utoaji damu, wenyeji hao waliionya serikali wakisema hawatataka kuona damu waliyojitolea inauzwa kwa wagonjwa hospitalini.

Wamesema, “tukitoa damu kwa hiari bila malipo, nayo isiende kuuzwa kwea wagonjwa tunataka wapewe bure, bila kutozwa ada yoyote.”

Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Afya wa Kenya, Wafula Nakhumicha alisema Serikali imeweka mikakati dhabiti ya kufuatilia damu yote iliyochangwa, ingawa hakugusia suala la mauzo ya hitaji hilo kwa wagonjwa waliopo Hospitalini.

Wanafunzi 25 wauawa Sekondari ya Mpondwe
UN: Zaidi ya watu 400 wameuawa Sudan Kusini