Klabu ya Kagera Sugar imeanza harakati za usajili wa kimyakimya na sasa inaelezwa iko kwenye hatua za mwisho za kunasa saini ya aliyekuwa nyota wa Mbeya City, Gasper Mwaipasi aliyeachana na timu hiyo kufuatia kushuka daraja msimu uliomalizika.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo zilieleza Mwaipasi amekubaliana masilahi binafsi na kupe- wa mkataba wa miaka miwili.

“Usajili wetu sio wa mbwembwe kama timu nyingine ndio maana huoni tukihusishwa sana kwa sababu mambo yetu tunafanya kwa uratatibu mzuri,” kimesema chanzo hicho.

Katibu Mkuu wa timu hiyo, Ally Masoud amesema licha ya wengi kuona ukimya wao ila haina maana kwamba hawajasajili mtu isipokuwa wanachokifanya ni kukamilisha dili hizo mapema iwezekanavyo ili ibaki kazi ya kuwatangaza tu kwa pamoja.

“Tunaendelea na usajili kama ilivyokuwa utaratibu wa kipindi hiki, wako ambao tumefikia makubaliano lakini wengine bado tunaendelea na mazungumzo na yatakapofikia sehemu nzuri watakuwa ni sehemu ya kikosi chetu kwa msimu ujao,” amesema.

Jonas Mkude atumika kuitisha Simba SC
Madini yapaisha mauzo ya bidhaa nje ya nchi