Viongozi wa upinzani wa Azimio la Umoja nchini Kenya, wamekaidi onyo la Serikali la kuharamisha maandamano yaliyopangwa kufanyika hii leo.

Viongozi hao, wamekuwa wakihimiza wafuasi wao kujitokeza na kushiriki maandamano hayo ya Jumatano, wakisisitiza kuwa yataendelea kama yalivyopangwa.

Jana (Jumanne Julai 11, 2023), Viongozi hao wakiongozwa na Raila Odinga na Kalonzo Musyoka walizindua saini za kidijitali kuunga mkono kuipinga serikali.

Wote kwa pamoja wamekuwa wakibainisha kwamba tayari watu milioni moja na laki mbili wameshatia saini kupinga Serikali iliyopo madarakani.

Jap Stam: Mikel Arteta ana mtihani mzito
Moto wateketeza nyumba Moro, mmoja afariki