Mamlaka za usalama na vyombo vya Habari nchini India, vimeripoti kuwa mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo, yamesababisha vifo vya takriban watu 41.

Waziri Mkuu wa jimbo hilo, Sukhvinder Singh Sukhu aliwaambia waandishi wa habari kuwa katika vifo hivyo 31 walikuwa ni wa eneo la Himacha Pradesh na wengine 10 katika eneo jirani la Punjab, na tukio hilo limethibitishwa na Waziri wa Mapato Brahm Shankar Jimpa.

Amesema, Himachal Pradesh imetoa dola 121,000 kwa shughuli za uokoaji na inapeleka helikopta sita kusaidia huku utabiri wa mvua zaidi ukitolewa katika majimbo yote mawili, ingawa Idara ya Hali ya Hewa ya India inasema inatarajiwa kupungua.

Hata hivyo, taarifa hiyo haikutaja idadi ya majeruhi wala kiwango cha madhara yaliyotokana na mvua hizo, lakini iliwasisitiza raia wake kuwa watulivu na waangalifu wakati taratibu za uokozi zikiendelea ili kutafuta miili na manusura.

FIFA yaiondolea vikwazo Zimbabwe
Mtenje Albano anukia Dodoma Jiji FC