Serikali imetaja sababu za kuanzisha majadiliano na kampuni ya DP World, kuwa ni pamoja na uwezo wake mkubwa katika uwezeshaji wa shughuli za bandari barani Afrika, Asia Ulaya, Amerika ya Kaskazini, lakini pia ile ya kusini na Australia.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa ujenzi na uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakati alipojitokeza hadharani mbele ya wahariri wa vyombo vya Habari kuzungumzia suala la uboreshaji wa Bandari unaotarajia kufanywa na Serikali ya Tanzaniana Dubai.

Waziri wa ujenzi na uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa.

Hata hivyo, wakosoaji wa Mkataba huo wanasema umeingiwa katika mazingira yaliyogubikwa na vitendo vya rushwa, ingawa hakuna ushahidi wowote uliowekwa hadharani, huku baadhi ya wanaharakati na wanasheria wakipinga mkataba huo na wanasiasa wa upinzani wameligeuza kuwa ajenda kuu ya kisiasa.

Hii inakuwa ni na mara ya kwanza kwa serikali kujitokeza kwa Wahariri wakati sakata la mkataba huo likiendelea kuwa mada inayojadiliwa kila kona, na katika kikao hicho Mbarawa aliambata na watendaji wake, na akabainisha utashi wa serikali kuwa hakuna ajenda yoyote iliyofichwa katika mkataba huo.

Raila anatafuta mbinu kupata nusu Mkate - Ruto
Mtu mmoja hawezi kuwapotosha werevu watatu - Mjengwa