Takriban Watu sita wamefariki na wengine 14 kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari wakati wakifanya mazoezi kandokando ya barabara eneo la Sabasaba Shule ya Msingi Lumala, lililopo Wilayani Ilemela jijini Mwanza.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Gideon Msuya amesema ajali hiyo imetokea hii leo Julai 22, 2023 majira ya asubuhi na kusema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hilo aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T476 DZL.

Amesema, “aliwagonga watu hao wa kikundi cha vijana kinachotambulika kwa jina la Adden hotel wakati wakifanya mazoezi ya kukimbia katika barabara ya sabasaba kuelekea Kiseke na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta dereva wa gari hiyo aliyekimbia baada ya ajali kutokea.”

Kufuatia ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala ametoa pole kwa familia za Marehemu na kutaka kuwaombea majeruhi ili wapone haraka, huku miili ya marehemu hao ikiwa imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa Sekou Toure.

Serikali yatangaza kusitisha malipo ya Walimu
Bruno Fernandes aukwaa unahodha Man Utd