Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika – EASTC, Dkt. Tumaini Katunzi amesema ipo changamoto ya kufanya baadhi ya maamuzi bila kuwa na Takwimu halisi, hasa kwa mtu mmoja mmoja na kwamba ili kuepukana na tatizo hilo kuna haja ya kuimarisha mifumo ya ufahamu juu ya masuala ya kitakwimu.

Dkt. Katunzi ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na Dar24 Media ofisini kwake hivi karibuni juu ya mambo mbalimbali ya uimarishaji wa mifumo ya data kwa kufanya uzalishaji, na utumiaji wa takwimu za kilimo kuwa wa kisasa.

Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika – EASTC, Dkt. Tumaini Katunzi.

Amesema, watu wengi hudhani Takwimu ni maamuzi ya Serikali kitu ambacho si sahihi kwani hata mtu mmoja mmoja anaweza kuwa na takwimu ambazo zinaweza kumsaidia katika kufanikisha mambo yake ya kila siku, ikiwemo njia zake za kiuchumi.

“Mfano Mkulima anahitaji kujua takwimu za masoko ya kibiashara, ajue takwimu za usafirishaji wa mazao, ajue takwimu za bei ya mazao na taarifa hizi kwa mkulima zitamsaidia sana kufanya maamuzi ya wapi auze mazao yake na ni kwa wakati gani.” amefafanua Dkt. Katunzi.

Aidha, Dkt. Katunzi amesema mfumo wa takwimu upo katika mpangilio halisi wa kukusanywa, kuchakatwa na kusambazwa kiutambuzi kujua ni wapi zinapelekwa na ni nani anayekwenda kuzitumia, ili iwe rahisi kufanikisha malengo husika kulingana na uhitaji.

Mafuta yapo nchi nzima, kasi usambazaji yaendelea - TAPSOA
Vituo vitapata Mafuta bila kuchelewa - TAPSOA