Idadi ya watu waliofariki kwa moto katika Mji wa Kihistoria wa Lahaina ulioko jimbo la Hawaii nchini Marekani, imefikia Watu 93, huku juhudi za uokoaji na kuwatafuta manusura zikiendelea .

Kwa mujibu wa Gavana wa Jimbo hilo, Josh Green amesema hata hivyo idadi hiyo ya vifo inaweza kuongezeka kwa kiasi kikubwa na kudai kuwa mamia ya watu bado hawajulikani walipo, huku wengine wakijazana katika makazi ya eneo la Maui baada ya kuokolewa na kuhamishiwa hapo kwa dharula.

Gavana Green alisema, “ni ngumu kwetu kuamini lakini ndiyo hali halisi imetokea, Moto huu umeleta maafa na hakika litakuwa ni janga baya zaidi la asili kuwahi kutokea Hawaii baada ya miaka mingi.”

“Tunaweza tu kusubiri na kusaidia wale wanaoishi. Lengo letu sasa ni kuwaunganisha watu tunapoweza na kuwapatia makazi, huduma za afya, na kisha kugeukia kujenga upya makazi watakayoishi,” alisema Gavana huyo.

Viongozi wa Dini wawaingilia kati mzozo ECOWAS, Jeshi la Niger
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 14, 2023