Serikali nchini, imesema inatoa shilingi milioni 77 kila mwezi, hivyo haitarajii Wananchi wanaokwenda kwenye Vituo vya kutolea huduma za afya kukosa dawa na kwamba wahusika wanatakiwa kupeleka Dawa sehmu huzika kulingana na mahitaji.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Majaliwa Wilayani Tandahimba, akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mtwara.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu pia alikagua na kuzindua mradi wa maji wa kata ya Kitama wenye thamani ya shilingi milioni 797, na kutumia fursa hiyo kuwasisitiza wananchi kuendelea kushirikiana kulinda vyanzo vya maji kwa sababu vikiharibika watakosa huduma hiyo muhimu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprica Mahundi alisema mbali na mradi huo pia Serikali inatekeleza mradi mkubwa wa maji wa Makonde wenye thamani ya shilingi bilioni 84 ambao utanufaisha wakazi wa Wilaya za Newala na Tandahimba, hivyo amewahakikishia wakazi upatikanaji wa maji ya uhakika na salama.

Liverpool yapigwa mweleka England
TAKUKURU yapewa agizo ubadhirifu fedha za Serikali