Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman amesema kuwepo kwa Taasisi ya Kujitathmini kwa hiari Afrika, katika masuala ya Utawala Bora ni fursa muhimu ya kusaidia kukuza uchumi na maendeleo endelevu nchini.

Othman ameyasema hayo ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar alipokutana na kufanya mazungunzo na ujumbe wa Taasisi hiyo kutoka Tanzania Bara uliongozwa na Katibu Mtendaji wake Bwana Lamau Mpolo.

Amesema, taasisi hiyo inapaswa kuelekeza juhudi zake kwa kuangalia kasoro na mapungufu kwenye masuala mbali mbali katika kuchangia kasi ya uwajibikaji ili kuimarisha uchumi na kuiwezesha nchi kuondoka mahali ilipo sasa na kuweza kusonga mbele kimaendeleo.

Othman amesema, masuala yanayohusishwa na taasisi hiyo ya kujitathimini katika suala la utawala bora yanagusa uwajibikaji kwa viongozi na wananchi ni muhimu hasa kwa vile yanazingatia maeneo yote ya kiuchumi na kimaendeleo kwa taifa na jamii kwa jumla.

Rais RFEF apangua uzushi wa mitandaoni
Ali Ramathan Mwirusi asaini dili Hispania