Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia – COSTECH, inaendelea kuimarisha mfumo wa ubunifu nchini kwa kuanzisha au kutoa usaidizi kwa vituo mbalimbali vya ubunifu, ili kuwafikia na kuwahuduma wabunifu kiurahisi.

Mkurugenzi Mkuu COSTECH, Dkt. Amos Nungu ameyasema hayo wakati kizungumza na Waandishi wa Habari na kudai kuwa mazingira wezeshi katika ubunifu ni pamoja na kuwa na mfumo stahiki unaosaidia wabunifu na bunifu nchini.

Amesema, “hii ni pamoja kuwapokea na kuwalea wabunifu, Sera na miongozo, mitaji, na mengineyo, huko nyuma tulitoa usaidizi kuanzisha kumbi za bunifu na tunaendelea kufanya nao kazi pamoja na kuwaita katika mafunzo.”

Hata hivyo, amesema mtafiti toka CoICT kwa Kushirikiana na wadau wengine kupata mitaji kwa ajili ya wabunifu kupata fursa ya mafunzo ya kijasiliamali kupewa mikopo nafuu inayoendana na mahitaji halisi.

TEHAMA waanzisha mradi kituo cha Taifa cha ubunifu
Serikali yatoa somo udhibiti wa Kemikali tabaka ozoni