Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amewataka wananchi kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa na watu wasio wema kuhusiana na ndege ya Rais, Gulf Stream – G550, kushikiliwa nchini Dubai.

Simbachawene ameyasema hayo hii leo Agosti 26, 2023 wakati akizindua Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali, katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere – JNICC, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene.

Amesema, “mtu anaweza kuzusha jambo na likawapotezea muda mwingi wananchi badala ya kufanya mambo ya maendeleo, kwa mfano uzushi kuhusiana na ndege ya Rais Gulf Stream (G550) kuzuiliwa Dubai.”

Aidha, Simbachawene ameongeza kuwa, “niwahakikishie kuwa ndege hiyo ipo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 VIP, jijini Dar es Salaam kwenye eneo ambalo Wakala wa Ndege za Serikali wanalitumia na yeyote anayepita barabarani ataiona.”

Mwinyi Zahera anajitafuta Coastal Union
Liverpool yakataa kumuuza Mo Salah