Serikali nchini, hii leo inazindua Ndege mpya ya mizigo  767-300F yenye namba za usajili 5H-TCO ikiwa na uwezo wa kubeba takribani uzito wa tani 58 na kuweza kuchochea shughuli za ukuaji wa uchumi.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege nchini – ATCL, Eng. Ladislaus Matindi imeeleza kuwa uzinduzi huo unafanyikq hii leo June 3, 2023 katika uwanja wa ndege JNIA.

Ndege hiyo ya mizigo ina uwezo wa kubeba takriban uzito wa  tani 58 ambapo hata hivyo Machi, 2023  ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG, ilifichua hitilafu katika upangaji wa bei ya ndege hiyo mpya ya mizigo.

Uwepo wa Ndege hiyo, utawezesha wawekezaji na wafanyabiashara ambao walilazimika kusafirisha mizigo yao kwa kutumia mashirika mengine ya ndege kutumia ATCL.

Ujenzi Mahakama ya Afrika haki za binadamu mbioni
Ugonjwa wa Marburg wamalizika Kagera - Serikali