Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu, limewahimiza wanachi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na vitendo vya ukatili Mkoani humo vinavyofanywa na Baadhi ya watu wasio na hofu ya Mungu.

Kauli hiyo imetolewa leo Agasti 27,2023 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Edith Swebe wakati wa sherehe za mavuno katika Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT Ushirika wa Tumaini Bariadi alipopata nafasi ya kutoa elimu ya Ukatili wa kijinsia.

Amesema, viongozi wa dini wanapaswa kutumia nyumba za ibada kukemea vitendo viovu pamoja na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia unafanywa na baadhi ya watu wasio na hofu ya Mungu huku akiwaomba wazazi kuongeza ulinzi kwa watoto ambao ndio waathirika wakubwa dhidi ya vitendo vya ukatili.

Kamanda swebe ameongeza kuwa, vitendo vya ukatili vinarudisha Nyuma maendeleo kwa makundi yote yanayofanyiwa ukatili katika jamii, huku akiwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo, ikiwa ni pamoja na kuiombea Nchi na Mkoa wa Simiyu kuendelea kuwa shwari.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 28, 2023
Ubora wa Chumvi: Waziri Mkuu atoa maagizo