Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, imeushauri uongozi wa Mabasi yaendayo Haraka – DART, kuanza kutumia teknolojia ya Smart Card, ili kupunguza kero ya upatikanaji wa tiketi kwa abiria, kudhibiti mapato na kuongeza idadi ya mabasi ili kukidhi mahitaji.

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya TAMISEMI, Justin Nyamoga ametoa ushauri huo wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge ya TAMISEMI ilipokagua miradi inayotekelezwa na DART katika Mkoa wa Dar Es Salaam.

Amesema,“ili kuepuka ulipaji fidia wa mara kwa mara wakati wakuongeza miundombinu tunaihitaji kuhifadhi eneo kubwa la kutosha hasa katika miji inayokuwa ili kuwa na maeneo kwaajili ya uendelezaji wa miundombinu hapo badae.”

Aidha, Nyamoga pia ametaka wakati wa ujenzi katika sehemu za makazi kuwe na umwagiliaji wa maji wa mara kwa mara, ili kupunguza kero na maradhi kwa wananchi.

Rais Samia kuzindua jengo Umoja wa Posta Afrika
Young Africans yaivutia kasi Al Merreikh