Wakala wa Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam – DART, umeomba radhi kufuatia ajali ya basi lake na na gari dogo aina ya Toyota RAV 4 iliyotokea eneo la Kisutu na kusababisha majeruhi kadhaa.

Akiongea na waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa DART, Dkt. Philemon Mzee amesema bado wanasubiri taarifa ya hospitali kujua ni watu wangapi wamejeruhiwa na hasara iliyopatikana.

Awali wakiongea katika eneo la ajali, baadhi ya mashuhuda tukio hilo wamesema chanzo cha ajali ni mwendokasi wa magari yote mawili, basi la DART na gari hilo dogo.

Aidha, uongozi wa DART umewataka madereva wote wakiwemo wa wakala huo na wale wa magari binafsi kuzingatia sheria za usalama barabarani, ili kuepuka ajali, vifo na hasara.

TANESCO yajipanga kuuza umeme nje ya nchi
Young Africans kuifuata Real Bamako alfajiri