Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO, limesema linatekeleza miradi kadhaa ya uzalishaji ambayo itasaidia kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa kila mwaka, ambapo zitapatikana Megawati 5000 hadi 6000 ifikapo 2025 na kuuza nje ya nchi.

Hayo yamesemwa hii leo Februari 22, 2023 Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wateja kutoka TANESCO, Martin Mwambene wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu majukumu na utekelezaji wa Taasisi hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wateja kutoka TANESCO, Martin Mwambene.

Amesema, uwezo wa uzalishaji wa umeme nchini ni Megawati 1,820, ambapo kwa sasa mitambo iliyopo inauwezo wa  kuzalisha Megawati 1,300 na kwamba TANESCO inatekeleza miradi kadhaa itakayosaidia kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa kila mwaka, ili kufikia lengo kusudiwa.

Muonekano wa Transfoma kubwa za kupokea na kufua umeme.

“Mradi wa Umeme wa Bwawa la Julius Nyerere upo asilimia 88, sasa hivi tumeanza kujaza maji ambayo yamefikia mita za ujazo 133 kutoka usawa wa Bahari, TANESCO tumefikiria mbinu za miradi mbadala ambayo itaongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme ikiwemo ya gesi na jua,”amesema Mwambene.

Aidha ameongeza kuwa, miradi ya uzalishaji umeme inaenda sambamba na miradi ya kusafirisha umeme, toka mradi wa JNHPP ambapo kuna njia ya itaanzia Rufiji mpaka Chalinze na tayari transfoma kubwa za Umba takriban sita zimepelekwa na zinasubiri kufungwa.

TCU yaimarisha mifumo viwango vya ubora
DART waomba radhi ajali Kisutu