Tume ya Vyuo vikuu nchini (TCU), imeimarisha mifumo yake ya ushauri na ukaguzi wa mara kwa mara wa kawaida na wa kushtukiza kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo kwa lengo la kuhakikisha kuwa elimu itolewayo hapa nchini inakidhi viwango vya ubora kitaifa, kikanda na kimataifa. 

Hayo yameelezwa na hii leo Februari 23,2023 na Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za tume hiyo kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita mbele ya waandishi wa habari, Jijini Dodoma.

Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa.

 Amesema, TCU imeweka utaratibu wa kuanzishwa na kuimarishwa mifumo ya uthibiti ubora ndani ya vyuo vikuu, ambavyo vimekuwa na utaratibu wa kujikagua, kujitathmini na kufanya marekebisho mbalimbali kwa kuzingatia miongozo ya uendeshaji wake.

 Aidha, Prof. Kihampa ameongeza kuwa katika kuwajengea uwezo wahadhiri na viongozi wa vyuo vikuu hususani utolewaji wa elimu ya chuo kikuu ,TCU imeendelea kuandaa na kuratibu mafunzo kwa viongozi,wahadhiri na maofisa wa vyuo vikuu vya umma na binfsi hapa nchini. 

Wanafunzi wa Elimu ya juu katika moja ya Mahafali.

Amesema, mwaka wa fedha wa 2022/23 Serikali imetenga kiasi cha Shilingi 6.4 Bilioni kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kichumi, kwa ajili ya kuimarisha uthibiti ubora na uhuishaji wa mitaala ya vyuo vikuu ambapo zaidi ya mitaala 300 ipo katika hatua mbalimbali za kufanyiwa mapitio, ili kuhuishwa kwa kuzingatia maoni ya wadau, kukidhi matarajio na mahitaji ya soko.

 Akizungumzia kuhusu suala la udahili wa wanafunzi wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2022/23, amesema ni 113.383 ikilinganisha na mwaka 2020/21 ambapo ulikuwa ni 87,934 ongezeko ambalo ni sawa na asilimia 28.9 likichagizwa na kuongezeka kwa fursa za masomo ya elimu ya juu na idadi ya wanafunzi wa kiwango hicho nchini. 

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 23, 2023
TANESCO yajipanga kuuza umeme nje ya nchi