Jeshi la Polisi nchini, limewataka wafugaji kufuata taratibu ikiwemo kupata vibali ama barua toka kwa
viongozi wa serikali za vijiji kabla ya kupeleka mifugo yao kwenye minada, ili kuondoa mashaka toka
kwa wakaguzi wa mifugo.

Hayo yamesemwa hii leo februari 22, 2023 na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia wizi wa Mifugo Nchini
Kamishna Msaidizi wa Polisi, Simon Pasua wakati akizungumza na Wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo katika mnada wa Duka bovu, uliopo wilaya ya Monduli mkoani Arusha.

Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia wizi wa Mifugo Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi, Simon Pasua.

Amesema, jeshi hilo linatoa elimu katika minada zaidi ya 530 iliyopo nchini na kwamba kupitia elimu hizo wafugaji wanaelimishwa taratibu za kufuata za namna bora ya kuuza mifugo yao, kuzingatia matumizi sahihi ya ardhi iliyotengwa kwa ajili ya kilimo, ili kuepusha migogoro.

Kwa upande wake Mfugaji, Kirayani Laizer amesema njia bora ya kudhibiti mifugo ya wizi ni kuweka zuio la mifugo isiyo na vibali toka kwa balozi au viongozi wa vijiji, kuingia minadani na kuwataka wafugaji wote kufuata taratibu.

Awali, Mfanyabishara wa mifugo, Babug Ngoti alitoa wito wa kuhakikisha wanafanya biashara yenye kuleta uwiano mzuri baina yao, wafugaji pamoja na serikali.

Basi la mwendokasi lapata ajali, lajeruhi
Raja Casablanca: Rais FMRF anatuhujumu