Basi la mwendokasi lililokuwa linatokea Kivukoni laparamia limepata jali ya kugongana na gari dogo eneo la Kisutu Jijini Dar es salaam, ambapo inadaiwa watu kadhaa wajeruhiwa.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa kuwa dereva wa basi la mwendokasi alikuwa anajaribu kulikwepa gari hilo dogo lililokuwa likikatiza barabara ya BRT bila kuwa na tahadhari.

Dereva wa Basi hilo alijitahidi kulikwepa gari hilo dogo lakini hakufanikiwa na kugonga ukuta wa jengo lililokuwepo upande wa kulia kisha kumkandamiza mtembea kwa miguu aliyekuwa pembezoni mwa barabara.

Endelea kufuatilia Dar24 Media kwa taarifa zaidi

Njaa yamkamatisha mtuhumiwa wa mauaji
Polisi yateta na wafugaji vibali uuzaji wa mifugo