Rais wa Marekani, Joe Biden amesema Rais wa Urusi, Vladimir Putin alikosea kudhani kwamba nchi yake inaweza kuishinda Ukraine na washirika wake wa Magharibi.

Biden ameyasema hayo, baada ya kufanikisha safari yake ya kwanza nchini Ukraine ikiwa ni siku chache kabla ya maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa uvamizi wa Urusi.

Rais wa Marekani, Joe Biden aliweka shada la maua kuwakumbuka Wanajeshi waliouawa katika kipindi cha miaka tisa tangu Urusi ilipotwaa eneo la Crimea. Picha ya Reuters.

Akiwa nchini humo, alikutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky na walitembelea kumbukumbu ya wanajeshi waliofariki katika kipindi cha miaka tisa tangu Urusi ilipotwaa eneo la Crimea na vikosi vyake vya wakala kuteka sehemu za eneo la mashariki la Donbas.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya White House, imeeleza kuwa Biden anathibitisha dhamira ya Amerika, mamlaka yake na uadilifu wa demokrasia ya Ukraine huku ikisema alisafiri kwa treni ya saa 10 kutoka Poland hadi kufika Kyiv kwa siri, kisha akarudi Poland.

Gerson Msigwa: Ahadi ya Rais ipo pale pale
Serikali yafuta ukomo kitambulisho cha Taifa-NIDA