Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kamishina Msaidizi wa Polisi Kaster Ngonyani amewataka wananchi wa Kijiji cha Lugonesi kilichopo Kata na Tarafa ya Mwese Wilaya ya Tanganyika kuacha tabia ya kuamini na kushiriki vitendo vya kishirikiana.

Wito huo, ameutoa Septemba 1, 2023 wakati alipofanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho, kufuatia uwepo wa mtu anayejiita kamchape au Lambalamba aliyefika katika eneo lao na kuwaaminisha Wananchi kuwa anaweza kubaini na kutoa uchawi huo hadharani, huku akiwachukulia wananchi fedha.

“Msikubali kudanganyika huyo ni tapeli mpuuzeni amekuja kwenu kuchukua fedha zenu tu, mtu huyu anafanya hivyo kinyume cha kisheria na taratibu za nchi kwani analeta taharuki ndani ya jamii hafuati utaratibu na masharti ya utoaji huduma wa tiba asili,” alisema Kamanda Ngonyani.

Kwa upande wao Viongozi wa kijiji hicho, maeneo jirani na Wananchi wameungana na kueleza kuwa suala hilo haliwafurahishi kwani limekuwa la udhalilishaji huku wakiomba mtu huyo azuiliwe kuendelea na shughuli.

Bodaboda wapewa somo kuepuka ajali, kifo
TANAPA yafafanua tukio Askari kujeruhiwa, yatoa onyo