Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi, Theopista Mallya amewataka Wanafunzi wa Sekondari ya kutwa ya Ilolo kupokea zawadi kwa watu wasio wafahamu, ili kupunguza na kutokomeza ukatili.

Kamanda Theopista ameyasema Agosti 31, 2023 wakati wa utoaji elimu wa Ushirikishwaji wa Jamii uliofanyika katika kata ya Ilolo iliyopo Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe.

Amesema, wanafunzi hao wanatakiwa kutoa taarifa za ukatili na zitafanyia kazi zitakapowasilishwa ili kuiweka  jamii katika hali ya usalama, huku akiwataka wanafunzi hao kutoa taarifa bila ya woga.

“Ulawiti, Ushoga, Ubakaji, Utoro Shuleni, Matumizi ya dawa za  kulevya, na kutojihusisha na mahusiano ya kimapenzi mkiwa wanafunzi hiyo haikubaliki inatakiwa mwanafunzi kuwa na kazi moja nayo ni kusoma tu, ili kuweza kutimiza malengo ya masomo yao,” amesema Kamanda Mallya.

Kwa upande wao, Walimu na Wanafunzi wamelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe  kwa kuendelea kushirikiana na wananchi katika suala la utoaji elimu kuhusu ukatili na usalama wa mali zao.

Tamko la NEMC uchimbaji dawa Safarini lawaibua Wadau
Kilimo cha Tumbaku, uvutaji Sigara vipigwe marufuku - Prof. Rogo