Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Kalala Mayele amesema anaamini bado ana nafasi ya kurejea Young Africans na kupokewa kwa furaha na mashabiki.

Mayele aliondoka Young Africans mwishoni mwa msimu uliopita 2022/23, akisajiliwa na Miamba ya Soka nchini Misri Pyramids FC, huku akiacha alama Jangwani kwa kuipa Ubingwa klabu hiyo mmisimu miwili mfululizo.

Mshambuliaji huyo amesema anafahamu kwa sasa hana uhusiano mzuri na Mashabiki wa Young Africans kutokana na kinachoendela katika Mitandao ya Kijamii, lakini ikitokea anarejea klabuni hapo kwa sasa anaamini atapata mapokezi mazuri.

“Pamoja na kwamba kumekuwa na vita kubwa juu yangu kwenye mitandao ya kijamii, bado naamini kwa asilimia 100% kwamba nikirudi Young Africans mashabiki watanipokea.

“Kitu ambacho nimejifunza Tanzania ni kwamba mashabiki wengi huwa wanajali maslahi yao na sio ya wachezaji.

“Kucheza misimu miwili ndani ya Young Africans ilikuwa ni furaha sana kwao, ila ilipofika hatua ya mimi kuondoka, watu walianza kunichukia bila sababu yoyote” amesema Mayele

Mshambuliaji huyo wa zamani wa AS Vita Club aliingia kwenye mgogoro na mashabiki wa Young Africans kufuatia andiko alilowahi kulichapisha katika Mitandao ya Kijamii akidai watu wa klabu hiyo wamemroga kwa kumtupia majini.

Rasha ampelekea tabasabu Kijana Mashilingi
Hali si shwari Manchester City