Kijana Nassibu Abdallah Mashilingi ambaye ni mlemavu wa miguu, amepata faraja baada ya kupatiwa mahitaji mbalimbali toka kwa Mkaguzi wa Polisi, toka Dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro, Michael Rasha.

Rasha ametoa msaada huo kwa kuambatana na Sajenti wa Polisi, Mwanaisha wa ofisi ya Dawati la Jinsia Wanawake na Watoto Wilaya ya Malinyi ikiwa ni kurejesha shukrani baada ya kufanikiwa kuwa mmoja ya Askari waliopandishwa cheo kutoka ngazi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kuwa Mkaguzi Kamili.

Kupandishwa kwake cheo kunatokana na ufanisi katika kazi mbali mbali za kuelimisha na kusaidia jamii, alizofanya mwaka 2023 na kupewa zawadi ya Pesa ambayo ameamua kurudisha kwa jamii anayoihudumia akisema, “kidogo tunachokipata ni chetu ndiyo sababu mimi nimeamua kuwasaidia wenye uhitaji.”

Mahitaji aliyokabidhiwa Nassibu ni pamoja na Unga, Mchele, Mafuta na sabani ambayo yatamsaidia kijana huyo ambaye anapata riziki kwa ugumu kutokana na changamoto ya hali yake.

Rais Young Africans afichua mapinduzi ya ubingwa
Mayele afunguka kurudi Young Africans