Rais wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Hersi Said, amefichua siri ya kufanya Mapinduzi ya Ubingwa kutoka kwa Watani zao wa Jadi ‘Simba SC’, waliokuwa mabingwa kwa Miaka minne mfululizo misimu mitatu iliyopoita.

Young Africans imekuwa na kikosi tishio katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara na kwenye michuano ya Kimataifa chini ya kiongozi huyo, ambaye aliingia madarakani miaka miwili iliyopita.

Hersi amesema kabla ya kufanya Mapinduzi ya Ubingwa, baadhi ya wadau wa Young Africans walikua hawamaini kama mpango huo ungeweza kufanikiwa, kutokana na ubora wa Simba SC kwa wakati huo.

Amesema alithibitu na kuwaaminisha wadau wa Young Africans katika safari ya mapinduzi ambayo kwa sasa yametamalaki kwenye soka la Tanzaania Bara, na hana budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufanikiwa katika hilo.

“Kuna watu walihisi ni ngumu kuuvunja ufalme wa Simba SC baada ya wao kubeba taji la nne mfululizo wa Ligi Kuu, nikawaambie subirieni niwaoneshe itakavyofanyika na sasa tupo hapa ila bado tuna malengo makubwa zaidi ya hapa” amesema Hersi

Mbali na kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo msimu huu 2023/24, Young Africans inawania taji la Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘CRDBFC’ kwa mara ya tatu mfululizo.

Mwishoni mwa juma hili Klabu hiyo Kongwe katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati itacheza mchezo wa fainali wa ‘CRDBFC’ dhidi ya Azam FC, Kisiwani Unguja ‘Zanzibar’, Uwanja wa New Aman Complex.

MALIMWENGU: Hofu yapelekea uchunguzi wa kifo ili wasife
Rasha ampelekea tabasabu Kijana Mashilingi