Polisi wa kulinda maadili wa Serikali ya Taliban, imewakamata watu sita kwa tuhuma za kupiga muziki katika Mkoa wa Kaskazini mwa Afghanistan wa Balkh, ambao walitenda tukio hilo wakati wa sherehe ya kifamilia katika mji wa Mazar-e-Sharif.

Hatua hiyo, inakuja baada ya mwezi Agosti 2021 Serikali ya Taliban liyorejea madarakani nchini Afghanistan kuweka marufuku kwa vyombo vya Habari kupiga aina yoyote ya muziki, huku Mkuu wa kukuza maadili wa mkoa huo, Sheikh Aziz al-Rahman al Muhajir akisema wamechukua hatua hiyo kwa kuwa muziki umepigwa marufuku.

Hivi karibuni, wamiliki wa kumbi za harusi nao waliagizwa kuepuka kupiga muziki, ikisema uhamasishaji wake ni aina mojawapo ya ufisadi, kupotosha vijana na kuleta uharibifu kwenye jamii.

Aidha, shughuli zote  zinazopingana na sheria za Kiislamu pia zilipigwa pia marufuku ikiwemo katika harusi na matukio kama hayo na tayari Wanamuziki wengi wa Afghanistan wametafuta hifadhi katika mataifa ya Magharibi, kutokana na misimamo hiyo.

Wafugaji waonywa kujichukulia Sheria mkononi
Wito: PAPU ianzishe mfumo anuani za makazi - Rais Samia