Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini Afghanistan ACAA imetangaza kufuta safari za ndege za kibiashara na kusema anga lake litatumiwa na ndege za kijeshi pekee hadi pale kutakapotolewa tangazo jingine. 

Nchini Afghanistan hali inaonekana kuwa tete hasa baada ya wanamgambo wa Taliban kuuzingira mji mkuu wa taifa hilo Kabul.

Mataifa mengi yameanza kuhamisha raia wao kutokana na hofu, huku mamlaka ya viwanja vya ndege nchini humo ACAA ikitangaza kufuta safari za ndege za kibiashara na kusema anga lake litatumiwa na ndege za kijeshi pekee, hadi pale kutakapotolewa tangazo jingine. 

Mapema leo mamlaka ya anga nchini Afghanistan, ACAA ilitangaza kufunga eneo linalotumiwa na wasafiri wa kiraia kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa kimataifa wa Hamid Karzai uliopo mjini Kabul.

Picha za video zilizosambaa zinaonyesha abiria waliofurika kiwanjani hapo wakivutana mashati, kila mmoja akitafuta angalau kijinafasi cha kujipitisha ili aingie kwenye ndege ya kijeshi iliyokuwa inawachukua watumishi wa ubalozi wa Marekani mjini Kabul.

Kulingana na ACAA, hatua hiyo inalenga kuzuia uporaji na uharibifu na kuonya abiria kutokimbilia uwanja wa ndege. Hata ndege zinazopitia Kabul nazo zimezuiwa.

Rais Dkt Mwinyi akutana na Balozi wa Oman nchini Tanzania.
Raia wa Afghanistan wakimbilia uwanja wa ndege