Mamia ya raia wa Afghanistan wameweka kambi katika uwanja wa ndege wa Kabul ili kukimbia nchi hiyo, hali hiyo imejiri mara baada ya wanamgambo wa Taliban kuutwaa mji huo.

Ripoti kutoka Afghanistan zinasema kuwa Wataliban wamechukua udhibiti kamili wa serikali, baada ya aliyekuwa rais, Ashraf Ghani kuikimbia nchi hapo jana.

Mpaka sasa mataifa mbalimbali yameanza kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha usalama wa raia wake, Rais wa Marekani Joe Biden ameagiza kikosi cha kijeshi kutoka Marekani kwenda kuhakikisha usalama wa Wamarekani.

Aidha Marekani imeondoka katika ubalozi wake mjini Kabul na kuwahamishia raia wake katika uwanja wa ndege ambao sasa umekuwa chini ya ulizi wake. Ujerumani pia imewaondoa raia wake kutoka Afghanistan.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linafanya kikao cha dharura leo kujadili hali hiyo nchini Afghanistan. Kikao hicho cha hadhara ambacho kitafuatiwa na kingine cha faragha vimependekezwa na Estonia pamoja na Norway.

Safari za ndege zafungwa Afghanistan
Askofu Gwajima ashikilia msiamamo wake ''nipo tayari kuacha Ubunge''