Askofu Mkuu wa kanisa la Ufufuo na Uzima lenye Mako Makuu yake, Ubungo Maji jijini dar es Salaam ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kawe (CCM), Josephat Gwajima ameendelea na msimamo wake na waumini wake kuwa kutochanjwa chanjo ya corona ambapo amesema kuwa Bunge likilazimisha, hatochanjwa.

Amesema hayo jana Agosti 15, katika ibada ya jumapili Askofu Gwajima amesema chanjo hiyo inayoendelea kutolewa nchini hazijafanyiwa utafiti wa kina kubaini madhara yake kwa wanaochanjwa na vizazi vijavyo.

“Wanaotaka nifukuzwe CCM watumie akili, kwa mfano tukichanja wote halafu kufikia 2025 watu wako hoi tutapigaje kampeni, bora wengine tubaki tusaidie kutetea chama chetu”.

“Kulikuwa na twitter inasambaa kwamba wabunge wote wachanjwe, baadae Ofisi ya Bunge ikakanusha nikasema hata ingekuwa kweli mie nisingechanjwa, ni heri kurudi hapa nyumbani, ubunge ni mzuri una heshima unasaidia wananchi lakini kunichanja hapana,” amesema askofu Gwajima.

“Sipingi chanjo ila hii haijafanyiwa tafiti za kutosha kwa maana hiyo nasema hapa hachanjwi mtu. Mimi sio adui yenu nalinda kizazi chenu kijacho na Tanzania yetu ijayo kwa nguvu zangu zote.”amesema askofu Gwajima.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Ofisi ya Bunge ilitoa ufafanuzi kuwa hakuna mbunge aliyelazimishwa kupata chanjo hiyo kwani chanjo ni hiari.

Raia wa Afghanistan wakimbilia uwanja wa ndege
Rais Samia kushiriki mkutano wa SADC Malawi