Kiongozi wa kijeshi wa Gabon, Jenerali Brice Oligui Nguema amesema raia wa nchi hiyo watapata fursa ya kuwa na katiba mpya kupitia kura za maoni, ikiwemo kanuni mpya za adhabu wakati wa uchaguzi.

Kiongozi huyo wa kundi la Maafisa wa Jeshi walionyakua madaraka Agosti 2023, dakika 30 baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa mshindi katika uchaguzi ambao walisema haukuwa wa kuaminika, aliyasema hayo mara baada ya kuapishwa kuwa Raisi wa mpito na Majaji wa mahakama ya kikatiba.

Katika hotuba yake, Nguema pia alipendekeza mageuzi na kuzipa kipaumbele benki za ndani na makampuni kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na kudai kuwa Wanasiasa walio uhamishoni wanakaribishwa kurudi na wafungwa wa kisiasa wataachiliwa.

Kiongozi huyo wa mapinduzi, alikuwa akishangiliwa na wafuasi wake katika sherehe zilizotangazwa kupitia televisheni, sherehe zilizobumiwa kuwaonyesha wanajeshi kama wakombozi wa jamii iliyokuwa imekandamizwa.

Abiria andikeni majina sahihi wakati wa Safari - SSP Didi
Bima ni muhimu kwa Uchumi wa Taifa - Rais Mwinyi