Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema anatambua umuhimu wa mchango wa sekta ya bima kwa uchumi wa nchi na kujikinga dhidi ya majanga mbalimbali.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati alipokutana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania – TIRA, Dkt. Baghayo Saqware na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amepongeza juhudi zinazofanywa na mamlaka hiyo kwa kuanzisha konsotia ya kilimo, pia nakuwataka kupanua wigo zaidi katika sekta za mifugo na uvuvi kwa kugusa wananchi wengi zaidi.

Naye, Kamishna Dkt. Saqware amewatambulisha Mabalozi wa Mamlaka hiyo kwa  Rais akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Injinia Zena Ahmed Said na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wanu Hafidh Ameir na Japhet Hasunga  ambao moja ya jukumu lao ni kutoa elimu ya uelewa wa Bima kwa Wananchi.

Jeshi laahidi Katiba mpya, kanuni za uchaguzi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 5, 2023