Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi amewataka wakandarasi kuzingatia ubora katika ujenzi wa majengo ya Ofisi za Serikali katika eneo la Mtumba jijini Dodoma, ili ukamilike kwa wakati.

Dkt. Yonazi ametoa rai hiyo wakati alipotembelea kujionea maendeleo ya ujenzi huo unaoendelea na kukagua baadhi ya majengo ikiwemo la Ofisi yake, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya TAMISEMI, Wizara ya Maji na Wizara ya Fedha.

Amesema, “dhamira ya Rais Samia ni kuona majengo haya yanakamilika kwa wakati na yawe na viwango vinavyotakiwa, bila kuwa na delays zozote ili kuhakikisha watumishi wote wanahamia haraka na kuendelea na utekelezaji wa majukumu yao na kuliletea Taifa maendeleo yanayotakiwa.”

Hata hivyo, alipongeza kwa hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo na kueleza kuwa, Serikali imejipanga kuhakikisha hakuna mkandarasi atakayekwama kwani Serikali haitaki kuona mikwamo katika ujenzi huu, huku akiwataka kutorudisha nyuma jitihada hizo.

Ukarabati Uwanja wa Mkapa kuiwahi AFL
Wahamiaji zaidi ya 3,000 wapewa uraia wa Tanzania