Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Ofisi ya Rais-TAMISEMI iendelee na utaratibu wa kubaini maboma yote kwenye sekta ya afya na elimu ambayo hayajakamilika kuhakikisha wanaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuyakamilisha kwani yametokana na bajeti zao.

Majaliwa ametoa maagizo hayo hii leo Septemba 7, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu Bungeni Jijini Dodoma, na kudai kuwa suala la ujenzi wa miradi ya elimu au afya ambayo inahusisha majengo ni mkakati ulioelekezwa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema, mkakati huo unatekelezwa kupitia fedha zinazopelekwa kutoka Serikali Kuu ambazo zinapelekwa kujenga majengo hayo kwa thamani ya jengo kutokana na makadirio waliyoyatoa, hivyo wanatakiwa wasimame ujenzi ukamilike kama ilivyokusudiwa.

“Uzoefu tulioupata wakati wa ukaguzi wa miradi hii, majengo yaliyotekelezwa kwa fedha toka Serikali Kuu yamekwenda kama yalivyo na ambayo hayakukamilika hatua kali zimechukuliwa. Kwa kuwa maboma mengi yanatokana na mipango yao na kushindwa kuyaendeleza, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha yanakamilika,“ amesema.

Serikali kusimamia Sheria zilizopo kuwalinda Wanyama
Mahakama yatupilia mbali hoja za Wapinzani