Katika kufanikisha utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na inayotekelezwa nchini Serikali ya Tanzania imenufaika na Shilingi bilioni 7.3 kutoka Serikali ya Norway na inatarajia kujengewa uwezo katika utekelezaji wa shughuli za mazingira.

Hatua hiyo imejiri baada ya Serikali hizo mbili kusaini Makubaliano ya kushirikiana katika shughuli za mazingira, hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amesema makubaliano hayo ni chachu ya utekelezaji wa jambo hilo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo na Waziri anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Anne Beathe Tvinnereim wakionesha nyaraka za makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Norway kuhusu ushirikiano katika hifadhi ya mazingira jijini Dar es Salaam.

Amesema, “makubaliano tuliyosaini leo yatasaidia katika miradi yetu ya kimazingira katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, nishati, maji, afya na ardhi na tuishukuru sana Serikali ya Norway, na sisi kama Ofisi ya Makamu wa Rais tunafurahi sana kwa miradi hii ambayo inakwenda kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi.”

Kwa upande wake Waziri anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Anne Beathe Tvinnereim na aliyesaini kwa niaba ya Serikali ya Norway amesema makubaliano hayo ni matunda ya uhusiano wa muda mrefu wa nchi hizi mbili.

Ronaldo hali tete, Messi apewa kipaumbele
Miquissone, Kramo wamchanganya Robertinho