Mabadiliko ya tabia nchi yanaendelea kuwa tishio na changamoto kubwa Zanzibar kutokana na kuendelea kuathiri shughuli za maisha ya wananchi kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman ofisinin kwake Migombani Mjini Zanzibar, wakati alipokutana na kuzungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Rick Shearn kuhusiana na masuala mbali ya ushirikiano.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman ofisinin kwake Migombani Mjini Zanzibar, wakati alipokutana na kuzungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Rick Shearn.

Amesema kwamba wananchi hasa wa Ukanda wa Pwani hivi sasa tegemeo lao kubwa la kiuchumi ni utalii sambamba na kuungana na serikali katika kutekeleza vipaumbele vyake vya mkiuchumi ikiwemo mpango wa uchumi wa bluu lakini mabadiliko hayo ya tabia nchi yamekua yakiathri sana ukanda huo.

Aidha, Othman ameongeza kuwa tatizo la mabadiliko ya tabia nchi limesababisha maeneo mengi ya visiwa vya Zanzibar kuingiwa na maji chumvi jambo ambalo linasababisha kiwango cha maji chumvi kuongezeka n ahata kuingia katika makazi ya wananchi na kuyataja maeneo kadhaa yaliyoathirika kuwa ni Nungwi, Jambiani na Paje.

Magaidi 11 wauawa, sita washikiliwa na Jeshi
Mkakati wa mapambano athari za ukame kuja na ripoti