Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji (UNCDF), Bi. Aine Mushi amesema Mkakati wa Tanzania kufaidika na miradi ya kuhamasisha matumizi endelevu ya ardhi hivyo kupunguza kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na athari zake, utakuja na ripoti ambayo itasaidia katika utekelezaji wake.

Mushi ameyasema hayo jijini Dodoma, kikao cha wataalamu cha kuhakiki rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Kupambana na Kuenea kwa hali ya Jangwa na Ukame, na kuongeza kuwa upo umuhimu wa kuona namna gani mkakati unashirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali zikiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wa maendeleo.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji (UNCDF) Bi. Aine Mushi akizungumza wakati wa kikao cha wataalamu cha kuhakiki rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Kupambana na Kuenea kwa hali ya Jangwa na Ukame chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa hali ya Jangwa na Ukame (UNCCD), Januari 25, 2023 jijini Dodoma.

Amesema, “Tunapowashirikisha wadau hawa tutaweza kujua ni kwa namna gani tunaingia kwenye mfumo wa bajeti ya Serikali na kwa kiwango gani cha fedha tunawezakutekeleza mkakati huu,” ameongeza Bi. Aine.

Kikao hicho, kimeshirikisha wawakilishi wa Wizara za kisekta wawakilishi wa washirika wa maendeleo, wawakilishi wa asasi za kiraia na wawakilishi wa sekta binafsi.

Mabadiliko tabia nchi yanathiri uchumi wa Wananchi: Othman
Rais Samia ateta na wadau Kilimo na Chakula