Waandishi wa habari wa Mkoa wa Pwani wamefanya ziara ya kutembelea kituo kikuu cha kupokelea Gesi cha Taifa Gas nchini kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam, kwaajili ya Mafunzo ya siku moja yakilenga kuwajengewa uwezo kuhusu umuhimu wa matumizi ya Gesi mbadala badala ya matumizi ya mkaa na Kuni kwa Taifa.

Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Taifa Gesi, Ambwene Mwakalinga akizungumza wakati wa ziara hiyo amesema Waandishi wa Habari waandike Habari za kuelimishe jamii kuhusu Faida na umuhimu wa matumizi ya gasi mbadala kwani asilimia 98.9 ya Watanzania bado wanatumia mkaa na kuni.

Amesema bado uelimishaji na uhamasisha wa jamii kuhusu matumizi ya nishati mbadala na athari za matumizi ya mkaa na kuni unahitajika na ziara hiyo ililenga kujifunza juu ya umuhimu wa matumizi ya nishati mbadala pamoja na kujionea shughuli mbalimbali za uchakataji wa Gesi kutoka katika kituo mpaka hatua ya mwisho ya kufika kwa jamii.

Aidha, amewataka Waandishi wa habari kuchukua hatua ili kusaidiana na Serikali kuokoa mazingira hasa katika kupunguza wimbi la ukataji miti hovyo kwasababu ya kuchomea mkaa na kuni na kwamba ili kufikia malengo ni vyema Serikali ikapandisha bei ya vibali vya uchomaji mkaa.

Ntibanzonkiza, Mayele wabadili kanuni TPLB
Mashabiki wachukulia poa ishu ya Ronaldo