Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wajasiriamali nchini kuendelea kubuni na kutengeneza nishati mbadala kwa kutumia rasilimali mbalimbali zilizopo nchini, ikiwemo vumbi la makaa ya mawe na mapumba za mahindi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jijini Dodoma huku akitoa wito kwa Watanzania kubadilika na kutumia nishati mbadala, ili kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.

Amesema, “tunataka watanzania waanze kutumia nishati mbadala, huu ndio muelekeo wa Taifa letu, tuendelee kubuni nishati mbadala kwa rasilimali zilizopo.”

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati Januari Makamba amesema wizara hiyo imejipanga kutumia makundi mbalimbali katika kuhamasisha Watanzania juu ya matumizi ya nishati mbadala.

TFF yatoa kauli kifo cha shabiki Uwanja wa Mkapa
Nyuki wamvamia mtu aliyetaka kumtapeli mpenzi wake