Polisi Kata wa Kata ya Hazina Wilaya Dodoma Mjini Mkoani Dodoma, Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi La Polisi, Verediana Mlimba ametoa elimu ya ukatili wa kijinsia katika kongamano la wadau wa afya ya akili lenye lengo la kusambaza uelewa wa afya ya akili.

Elimu hiyo, ilitolewa na Mlimba kwa jamii katika Hospitali ya Taifa ya Taifa ya Akili mirembe iliyopo jijini Dodoma, ikilenga kuwaelimisha juu ya masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kukabiliana na uhalifu.

Katika Semina hiyo, Mlimba aliwataka wadau wa afya ya akili kushurikiana na Jeshi la Polisi katika kukemea vitendo vya ukatili na mauaji vinavyofanyika katika jamii, ambavyo vinasababishwa na kukosekana kwa utimamu wa afya ya akili.

Aidha, ameeongeza kuwa kukosena kwa utimamu wa afya ya akili kwa binadamu kunachangia kuwepo kwa matukio ya uhalifu ikiwemo, kujiua, kufanya mauaji kwa kujichukulia sheria mkononi pomoja na matukio mengine ya ukatili ambayo nikinyume na taratibu na sheria.

Van Dijk aongezewa adhabu England
Wananchi endeleeni kuiamini Serikali - Majaliwa