Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Malinyi, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, ASP. Shangwe Mlela amewataka waumini wa Kikristo kutumia mafundisho ya dini kama silaha ya kurekebisha maadili ya familia zao na jamii.

ASP Mlela ameongea hayo wakati alipohudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa la Roman Catholic, Kijiji cha Biro Akilichopo Tarafa ya Ngoheranga Wilaya na Mkoa wa Morogoro na kuitaka kuwa na hofu ya Mungu ili kuondoa uhalifu.

Amesema, “Viongozi wa dini wanatakiwa kukemea mila na desturi zisizofaa ambazo zinaletwa katika jamii zetu, ninyi mna nafasi kubwa katika kuzuia mila hizi zinazochangia uwepo wa viashiria vya ukosefu wa maadili na uwepo wa uhalifu.”

Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Michael Rasha Polisi kata wa eneo hilo naye amewataka waumini hao kushirikaiana na Jeshi la Polisi kulinda watoto, ili wasijiingize kwenye makundi yasiyofaa, ikiwemo matumizi wa dawa za kulevya na wizi.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 11, 2023
Idadi vifo vya Tetemeko Morocco yazidi Watu 2,000