Serikali nchini, imewataka Mafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Mitaa na watendaji wa jiji la Dodoma kuzingatia mwongozo wa matumizi thabiti ya Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi, kwani ni msingi katika kuwezesha ukuaji wa Sekta mbalimbali za Kijamii, Kiuchumi, maangalizo ya kiusalama na tahadhari za majanga Mbalimbali

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Alhaji Jabir Shekimweri katika ufunguzi wa mafunzo ya kujenga uwezo kuhusu mfumo wa anwani za makazi kwa Maafisa hao Jijini Dodoma na kudai kuwa yana fursa adhimu ya kufahamu masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi.

Amesema, “tumejiridhisha kwamba Mafunzo haya yanaumuhimu kipekee ili dhamira njema na maono ya Mheshimiwa Rais wetu kuwa na anwani za makazi na faida ambazo zimetajwa hapa ziweze kupatikana Kwa mapana yake na zoezi lenyewe liweze kuwa endelevu.”

Aidha, Shekimweri ameongeza kuwa kwa kutumia simu ya mkononi kupata huduma yoyote kupitia mfumo wa anwani za makazi kihuduma licha ya zoezi hilo kuwepo kwa miongo yote toka Nchi ipate uhuru, lakini sensa ya mwaka 2022 ilikuwa ni sensa ya kipekee.

“tulifanya zoezi na kutambua tupo Watanzania Milioni 61 na tukatambua pia majengo na mtakumbuka Rais Dkt. Samia wakati akizindua taarifa Ile ya awali ya sensa tarehe 31 Oktoba mwaka Jana (2022), alituambia Tanzania bara kuna majengo million 13.9 na visiwani kuna majengo 440,451”. Amesema Shekimweri.

Kwa upande wake Afisa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anord  Mkude amesema ni muhimu kila mtu kufahamu maana ya anuani za makazi, mfumo wa anwani za makazi, muundo wa anwani za makazi na mahusiano ya Posti Kodi, jina la barabara na namba ya nyumba au namba ya anwani.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 15, 2023
Waliofariki kwa mafuriko Libya wafikia 6,000